Luke 24:13-18

13 aIkawa siku iyo hiyo, wanafunzi wawili wa Isa walikuwa njiani wakienda kijiji kilichoitwa Emau, yapata maili saba
Maili saba ni kama kilomita 11.2.
kutoka Yerusalemu.
14Walikuwa wakizungumza wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotukia. 15 cWalipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Isa mwenyewe akaja akatembea pamoja nao, 16 dlakini macho yao yakazuiliwa ili wasimtambue.

17Akawauliza, “Ni mambo gani haya mnayozungumza wakati mnatembea?”

Wakasimama, nyuso zao zikionyesha huzuni.
18 eMmoja wao, aliyeitwa Kleopa, akamuuliza, “Je, wewe ndiye peke yako mgeni huku Yerusalemu ambaye hufahamu mambo yaliyotukia humo siku hizi?”

Copyright information for SwhKC